Hofu kubwa na wahaka mzito umewagubika viongozi na wananchi wa Israel baada ya jeshi hilo kushambulia askari wa kikosi cha Hizbullah.
Jeshi la Israel limetumia helkopta kuvamia msafara wa kikosi cha askari wa hizbullah na kuua askari sita,
Katika kitongoji kiitwacho mazraat ammar, iliyopo katika ardhi ya Syria karibu na milima ya Golan, ambako askari hao wa Hizbollah wamepadhibiti kwa ajili ya kulinda amani na kuilinda serikali halali ya Bashar asad wa Syria.
Askari waliokufa kishahidi katika shambulizi hili ni:
- Kamanda Mohammad Ahmad Issa, maarufu kama “Abu Issa” mwenye mke na watoto wanne.
- Jihad Imad Mughniyah maarufu kama “Jawad” huyu ni mtoto wa mkuu wa majeshi wa Hizbullah, Shahidi al haj Imad Mughniyah ambaye aliuawa katika shambulizi lililofanywa na jeshi la Israel.
- Abbas Ibrahim Hijazi, maarufu kama “Sayyed Abbas” ameona na anawatoto wanne.
- Mohammad Ali Hasan Abu Hasan maarufu kama “Kazim”.
- Ghazi Ali Daui maarufu kama “Daniel”.
- Ali Hassan Ibrahim maarufu kama “Ihab”.
Shambulizi hilo lililofanywa na Israel limeleta hofu isiyokifani hata katika safu ya wanajeshi wa nchi hiyo ambapo mmoja kati ya makamanda wa jeshi hilo alisema kuwa:” tunayakini kuwa Hizbollah lazima watalipa kisasi.”
Lakini mpaka sasa hakifahamiki kisasi hicho kitakuwaje na kitakuwa lini na kitatokea pande gani.
Mmoja kati ya makamanda wa Hizbullah alisikika akisema kuwa:”Shambulio hili halitaachwa bila ya kisasi”.
Tukio hili limetokea katika wakati ambao siku chache tu zilizopita kiongozi mkuu wa Hizbollah Sayyid Hasan Nasrullah alitanganza kuwa ikiwa Israel itaanzisha vita dhidi ya Hizbullah basi jeshi la Hizbullah litapambana na kupeleka majeshi yake mpaka ndani ya ardhi ya Israel.
Kikundi cha Hizbullah ni kikundi cha wanajeshi wa kishia kinachojitolea kulinda nchi ya Lebanon dhidi ya mashambulizi ya Israel, kikundi hiki kina miliki silaha za kisasa na makombora ya masafa ya kati na masafa mafupi, kikundi hiki kinapata udhamini kutoka Jamhuri ya kiislamu ya Iran na Syria pia kinapata mafunzo ya kijeshi kutoka kwa kikosi maalum cha jeshi la Quds la Jamhuri ya kiislamu kilicho chini ya Qasim Suleimani, kamanda wa Iran anayeogopewa zaidi na Marekani kutokana na uwezo wake katika kupanga mashambilizi na kuwaandaa makomandoo wenye mbinu pekee za kivita.
Ikumbukwe kuwa mnamo mwaka 2006, kikosi cha Hizbullah kililishinda jeshi la Israel baada ya jeshi hilo kufanya mashambulizi mazito kwa lengo la kuliangamiza kundi hilo la Hizbollah na kuokoa mateka wake, vita hivi viliipatia Israel hasara kubwa na kupelekea wanajeshi wake wengi kuuawa na hatimaye kwa mara ya kwanza katika historia jeshi la nchi hiyo lilinyoosha mikono na kuomba sulhu, hali iliyopelekea kushuka na kuporomoka heshima ya nchi hiyo ambapo waumini wengi wa ya Kiyahudi na kikristo wanaamini kuwa ni nchi ya Mungu.
Waziri mambo ya nje wa Jamhuri ya kiislamu ya Iran Mohamamd Javad Zarif amelaani shambulizi hilo lilifanywa na Israel na kuliita kuwa ni shambulizi la shambulizi la kigaidi.